Search This Blog

November 14, 2012

POLE SANA DIAMOND: DIAMOND AELEZEA KILICHO SABABISHA AJALI YAKE..!!!Kupitia tovuti yake ya ThisisDiamond.com msanii huyo ameandika:
"Tarehe 10 ya mwezi wa 11 siku ya juma mosi ni moja ya siku ambazo sitozisahau maishani mwangu.
Baada ya kumaliza majukumu yangu ya kila siku, nilikwenda masaki kumwona mmoja wa jamaa zangu wa karibu nikiwa na Blogger wangu Bestizzo pamoja na mwanafamilkia ya wasafi Dumi(Dancer) Mishale ya saa moja hivi nikiwa maeneo ya masaki karibu na kona ya msasani nilipata ajali ambayo haikuwa kubwa sana ingawa imesababisha uharibifu kwa kiasi kikubwa, Kama mjuavyo barabara ya msasani ni ndogo na gari huwa haziko katika mwendo wa kasi... ghafla dereva wa pikipiki alikatisha mbele yangu na katika kujaribu kumkwepa nikagonga gari ndogo aina ya Rav 4 ambapo ilisababisha dereva wa pikipiki kuanguka katikati ya gari zote mbili. Hiyo ndio hali halisi ya ajali niliyokutana nayo jumamosi iliyopita.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutunusuru wote bila majeraha makubwa zaidi ya maumivu tu ya hapa na pale."

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...