Search This Blog

November 10, 2012

‘Kaseja Njoo Yanga hakuna Majungu’....Navyompenda Kaseja timu Yeyote Atakayokwenda Ntakuwa Mfuasi Wake.....


Juma Kaseja mlinda mlango wa Simba
Na Mwandishi Wetu
MLINDA mlango nambari wani Bongo, Juma Kaseja ambaye juzikati ameingia kwenye lawama baada ya timu yake ya Simba kupigwa bao  2-0 na Mtibwa Sugar ya Morogoro, anaweza kupata namba katika Klabu ya Yanga ya Jangwani.
Wakizungumza na Udaku Spoti juzi Alhamisi, baadhi ya wanachama wa klabu hiyo ya Jangwani, walimtaka Kaseja kuachana na Simba na kutua Yanga wakidai hakuna lawama za ‘kijinga’ wala majungu.

“Kaseja kafungwa juzi na Mtibwa, lawama zinatupwa kwake, kwani alicheza peke yake uwanja mzima? Sisi tunamwambia Kaseja kama vipi aje Yanga, hakuna lawama wala majungu kama Msimbazi, sisi tukifungwa tinakaa na kujiuliza kwanza,” alisema Rashid Mkondolele, Mwanayanga wa Ilala, Dar.
Mwanachama mwingine wa Jangwani, Simba Abdallah ‘Kitope’ alimtaka Kaseja kuachana na timu hiyo isiyokubali kushindwa na ajiunge Yanga ambako kwa sasa ni mwendo mdundo.

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...