Search This Blog

November 14, 2012

JE WAJUA NAFASI AMBAZO MHESHIMIWA ABDULRAHMAN KINANA AMBAZO AMEWAHIKUSHIKA? PATA KUZISOMA UJUE KWANINI NI HERO WETU....PONGEZI NYINGI ZIMWENDEE!!!!!!


Pichani ni Mwanajeshi Mkakamavu wa zamani wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Arusha Mjini, Waziri wa Zamani w
a Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Katibu Mkuu Mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akionekana Mtanashati katika Vazi lake la Uspika wa Bunge la Afrika Mashariki.

Picha hii ilipigwa Mwaka 2001 wakati Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa kuwa Spika wa Kwanza wa Bunge la Afrika Mashariki, nafasi ambayo aliishika kwa Muda wa Miaka mitano.

Kinana pia anatajwa kuwa Meneja wa Kampeni wa CCM katika Uchaguzi wa Mwaka 1995 uliomuingiza Madarakani Rais Benjamin William Mkapa na pia Mwaka 2010 katika Uchaguzi Mkuu uliomuingiza Madarakani Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri ukishirikiana na blog ya Tanzanite glamour unampongeza Ndugu Abdulrahman Kinana kwa Uteuzi alioupata katika nafasi husika na unamtakia kila la Kheri katika Majukumu yake Mapya.

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...