Pichani ni Rais Benjamin William Mkapa akikumbatiana na aliyekuwa Mpinzani wake katika Kinyang'anyiro cha Kupata nafasi ya Kugombea Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya Yeye (Mkapa) kutangazwa Mshindi kwenye Kura za Marudio kat yake na Kikwete.
Picha hii ilipigwa Mwaka 1995 Huko Makao Makuu ya CCM Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wa Uteuzi wa Mgombea Urais kupitia chama hicho.
Siku kama ya leo miaka 74 iliyopita Rais wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Benjamin William Mkapa alizaliwa huko wilayani Masasi, kusini mwa Tanzania.
Mzee Mkapa ni Mhitimu wa Shahada ya Elimu ya Juu kutoka katika Chuo Kikuu cha Makerere Nchini Uganda ambapo zaidi alijihusisha na Fani ya Fasihi ya Lugha ya Kingereza na Uandishi akisoma Darasa Moja na Nguli wa Fasihi wa Kenya, Profesa Ngugi wa Thiongo.
Mkapa ameshika nafasi Mbalimbali Serikalini kuanzia Uhariri wa Magazeti ya Serikali, Uandishi wa Hotuba Ikulu chini ya Rais Julius K. Nyerere ambaye alikuwa Mwalimu wake huko katika Shule ya St. Francis Pugu, Jijini Dar es salaam, Afisa Mipango huko Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kabla ya kushika nafasi nyeti ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ukurasa wa Watanzania Mashuhuri unapenda kuchukua Fursa hii kumtakia Kila la Kheri Rais Mkapa katika maisha yake na pia kumpongeza kwa kufikisha Miaka hiyo ambayo ni mingi sana kwa Kizazi cha Tanzania.
Mola aendelee kumpa Busara zaidi zenye kulingana na Umri wake na atujaalie sisi Watanzania tufuate yale mema yaliyotendwa naye.
Happy Birthday Rais Benjamin William Mkapa.

No comments:
Post a Comment
ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION
Note: Only a member of this blog may post a comment.