Search This Blog

November 13, 2012

MKUTANO MKUU WA CCM: HUKUMU NZITO KUTOLEWA LEO


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha wajumbe wa NEC Dodoma, kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama.
Stori: Mwandishi Wetu, Dodoma
HUKUMU nzito inatarajiwa kutolewa leo  na Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na madai kwamba kuna kiongozi wa ngazi ya juu amekuwa akimwaga fedha ili kujiwekea njia ya kuteuliwa siku zijazo agombee urais kupitia chama hicho.
Wakati madai hayo yakiwa yamesambaa kulikuwa a kila dalili kwamba Rais Jakaya Kikwete alitarajiwa kuchaguliwa kushika wadhifa huo baada ya Jumamosi iliyopita Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (Nec) kumchagua kwa kishindo kugombea nafasi hiyo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Taifa wa CCM, Nape Nauye aliyezungumza akiwa Kizota mjini hapa,  alisema wajumbe wa Nec walipitisha jina moja tu la Kikwete kuwania nafasi hiyo ya juu katika chama hicho kikongwe nchini. “Alipitishwa kwa kishindo na Nec hiyo ilikuwa dalili nzuri kwa kiongozi wetu kuendelea kuongoza chama chetu,” alisema Nape.
Ushindi wa Kikwete  umepokelewa kwa shangwe na wanachama wa chama hicho na kuwaumbua wale waliokuwa wanadhani kwamba kofia mbili za urais na uenyekiti wa CCM vingetenganishwa.
Akifungua mkutano huo Jumapili iliyopita Kikwete aliwataka  viongozi waliochaguliwa kuziba nyufa za uchaguzi.
“Uchaguzi umekwisha, jengeni chama, zibeni nyufa za uchaguzi na pokeeni kauli mbiu ya mkutano huu ambayo inasema umoja ni ushindani,” alisema Kikwete.
Aidha, Nec pia ilipitisha jina la Philip Mangula kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akapendekezwa awanie nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Visiwani ambapo mkutano mkuu wa chama hicho, ulitarajiwa kuwapitisha jana

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...