Search This Blog

October 24, 2012

UCHAGUZI CCM NOMAAAAAAA......


Stori: Mwandishi Wetu
UCHAGUZI ndani ya Chama Cha Mapinduzi ‘CCM’ ni noma ambapo sasa makundi yamejiweka wazi katika nia ya mwelekeo wa ushindi.
Edward Ngoyai Lowassa
Uchunguzi umeonesha kuwa katika chaguzi za chama hicho miaka ya nyuma, mwaka huu ni kiboko kwani wengi wanaamini ndiyo utatoa dira ya ushindi au anguko la chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015. Aidha, vita vimekuwa vikali kwa sababu 2015 ndiyo mwaka ambao CCM itatoa mgombea mwingine wa urais kwani JK atamaliza awamu yake ya pili ya uongozi wa nchi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), Sophia Simba, wakati akiingia katika ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa Jumuiya hiyo.
Uchunguzi umezidi kubaini kuwa vita kubwa ipo kambi kwa kambi na si kwa wagombea wenyewe. Ushindi wa kambi moja ndiyo anguko la kambi nyingine na ndiyo ushindi wa mwaka 2015 kutoa mgombea wa urais wa chama hicho tawala kwa sasa.
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, (aliyekaa), akitulizwa hasira na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwkezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu, wakati wa kikao cha uchaguzi mkuu wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, UWT, kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango Dodoma Jumamosi Oktoba 20, 2012.
Mfano ile ‘sinema’ ya vigogo wa CCM, Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania ‘UWT’, Sophia Simba na Mbunge wa Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji wakati wa mkutano wa uchaguzi wa umoja huo mwishoni mwa wiki iliyopita imefika hatua ya kutikisa Ikulu na wengi wanasema tafrani ile ilitokana na vita ya kambi na si vinginevyo.
Shy-Rose Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku akitulizwa na mjumbe mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba.
Mara baada ya kutokea purukushani ndani ya ukumbi wa uchaguzi mjini Dodoma kabla ya kuchaguliwa mwenyekiti wa UWT, wana usalama walifikisha taarifa Ikulu na rais akajadiliana na washauri wake.
Madai haya yanathibitishwa na JK mwenyewe alipokwenda kufunga mkutano huo Jumatatu iliyopita ambapo alisema kwamba anawapa pole wote kutokana na misukosuko iliyotokea siku hiyo ya uchaguzi.
“Nyote nawapa pole kwa misukosuko iliyowakuta maana uchaguzi si kazi ndogo hasa siku hizi ambapo kuna mambo mengi na mengine yanasikitisha hata kuyasema yanatia aibu,”  alisema Kikwete.
Wakati huo huo, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, UV-CCM ambao umepata viongozi wa kitaifa kupitia mkutano mkuu wao uliofanyika juzi mjini Dodoma, inaelezwa pia kuwa walioshinda ni wenye mwelekeo wa vita ya makundi kwa mapambano ya mwaka 2015.
Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ndiye anayetajwa kupeta katika chaguzi hizo huku wengine wakisema kambi yake imekuwa na nguvu na kupanuka kwa sasa kuliko miaka miwili nyuma japokuwa kuna kambi inayotajwatajwa kuwa ni ya Bernad Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
SOURCE: GP

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...