Search This Blog

October 19, 2012

MWANZO MGUMU DIAMOND ANAWASHAURI MSIKATE TAMAA, ANGALIA VIDEO YAKE YA KWANZA AKIWA HAJAWA SUPER SUPER!!!!DIAMOND FT. FATMA & ROMY JONES - TOKA MWANZO


MANENO YA DIAMOND: Daah! Maisha ni safari ndefu sana ndugu zangu na hakuna anae jua wapi anaelekea wala aliyezaliwa anajua chochote,siku zote mwanzo huwa mgumu sana ukiongeza na maneno ya watu ya kukukatisha tamaa basi ndio unazidi kuyaona Maisha magumu na kukata tamaa na kujiona huwezi kabisaaaa!... Mimi wakati naanza muziki nilikutana na mambo mengi sana ya kukatisha tamaa lakini siku zote sikuchoka kumuomba Mwenyezi Mungu anisaidie na kuzidisha juhudi kila dakika..... 
Naitumia nafasii hii pia kuongea na wasanii wachanga wanaochipukia kwenye sanaa ya muziki wasikate tamaa na hizi ni kama nguzo zinazoweza kukufanya angalau kupiga hatua.....Kwanza kabisa ni Maombi,Uvumilivu,Juhudi,Ubunifu na Heshima inahitajika sana.....Ukiangalia Video yangu ya Toka mwanzo na hiyo ya Mawazo niwazi kabisa utajionea utofauti mkubwa sana na utakubaliana na mimi ama kweli MAISHA NI SAFARI NDEFU SANA. 

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...