Search This Blog

September 24, 2012

SO HAPPY FOR SAJUKI AND WASTARA MUNGU NI MWEMA SAJUKI KAPONA SASA NA KUFUNGA NDOA, UVUMILIVU MTAMU JAMANI!!!!!HAHAHAHA HAWA NI WANANDOA NI MBWEMBWE TUU!!!!

Na Imelda Mtema
MASTAA wa filamu Bongo ambao ni wanandoa, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ na Wastara Juma hivi karibuni waliwaacha watu hoi kufuatia vituko walivyokuwa wakivionesha, Ijumaa Wikienda liliwanasa kwenye shughuli.
Wawili hao walionesha vituko hivyo kwenye harusi ya mdogo wa Wastara aitwaye Latifa Juma iliyofanyika mwishoni mwa wiki, Tabata jijini Dar.

Katika sherehe hiyo, Wastara aliamua kuweka matatizo yao pembeni na kuanza kukata nyonga kwa staili iliyowaacha hoi maharusi pamoja na watu wengine waliokuwepo kwenye ‘mnuso’ huo. 
Achilia mbali hilo, Sajuki naye alipoingia ukumbini hapo aliingia kwa staili ya kucheza kiduku huku mkononi akiwa ameshika kimfuko cha bisi ‘pop corn’.
Vituko havikuishia hapo kwani kuna wakati Wastara alipotakiwa kufika mbele kukata keki, Sajuki alimfuata kwa nyuma na kumshikia gauni lake refu kama mpambe wake na keki ilipokatwa alichukua kipande na kukila hata kabla ya maharusi.

Mpaka wawili hao wanaondoka ukumbini hapo, walikuwa wameacha gumzo kutokana na matukio yao ambayo yaliifanya sherehe hiyo ifane. 
SOURCE: GP

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...