Search This Blog

September 20, 2012

I-View kurekodi video mpya ya Diamond


KAMPUNI ya I-View Studios ya Dar es Salaam imeshinda mchakato wa kurekodi video mpya ya msanii mahiri, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambayo usaili wake utafanyika kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge, jijini Jumamosi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya One Touch Solutions, Peter Mwendapole, alisema I-View imepata nafasi hiyo kutokana na kiwango kikubwa cha video kadhaa ilizoandaa, lakini pia vifaa ilivyonavyo na uwezo wa wafanyakazi wake.
“Siku zote kila mtu anaangalia kitu kizuri, Diamond ametaka kufanya mapinduzi katika tasnia ya muziki, lakini kufanya mapinduzi kunahusisha vitu vingi, tungo zake yeye kama msanii, studio anayorekodia, watu watakaoshiriki kwenye video yake na kampuni itakayorekodi video pia, lakini mwisho wa siku I-View chini ya Raqey Mohamed ndiyo imeshinda nafasi hiyo.
“Raqey anafahamika kwa kazi zake pamoja na kurekodi matangazo mbalimbali ya televisheni na picha mnato, lakini pia video za wasanii Taznim ya ‘Kwasakwasa’, ‘Utanikumbuka’ ya Suma Lee ni baadhi ya kazi ambazo zinaonyesha uwezo alionao, lakini pia Diamond na timu yake tumeweza kuona vifaa vipya na vya kisasa ambavyo Raqey anavyo kwa sasa na hakuna kwa Afrika Mashariki na Kati,” alisema.
Kwa upande wake, Raqey ambaye ni Mkurugenzi wa I-View, alisema anahitaji kuifanya kazi hiyo kuwa tofauti ili kusukuma mbele sekta ya mawasiliano na muziki kwa ujumla.
“Sisi kama I-View tunafurahi kufanya kazi na Diamond, ni msanii mzuri na mkubwa ambaye kazi zake zinaonekana, hatutamuangusha na mashabiki na wasanii wengine wasubirie kazi itakapotoka,” alisema.
I-View pia watashiriki katika mchakato wa kupata watu watakaonekana kwenye video hiyo ambayo ni kwa mara ya kwanza nchini kutafanywa usaili wa washiriki.
Usaili huo utafanyika Jumamosi Ukumbi wa Nyumbani Lounge ambao unamilikiwa na mwanamuziki Lady Jaydee. Majina ya majaji wataochuja yanatarajiwa kutangazwa leo.
SOURCE: TD

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...