Search This Blog

April 10, 2012

HESHIMA ZA MWISHO ZILITOLEWA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI NANINGEPENDA KUWASHUKURU WOTE WALIOWEZA KUFANIKISHA MSIBA HUU KUWA WA AMANI BILA KUISAHAU SERIKALI YETU NA VIONGOZI WAKE.

Tanzanite Glamour inapenda kutoa shukrani kwa wale wote walioguswa na msiba wa kaka yetu marehemu Kanumba, mungu awe nanyi na kuwaongezea. Watanzania wameonyesha upendo wa ajabu katika kipindi hiki kigumu kwa familia ya Mzee Kanumba. Ningependa binafsi kuishukuru serikali yetu ya Jamhuri Wa Muungano kwa yote waliyoyafanya katika familia ya Kanumba. Umoja umeweza kuwa nguvu katika kufanikisha Mazishi ya kaka yetu. Nawashukuru wote walioweza kututumia picha za matukio kwanzia msafara hadi leader's club na makaburini. Nawashukuru Cloud fm kwakutuonyesha msiba live,blog ya Dj Choka na Bongocelebrity kwakuturushia matukio tulio nje ya nchi. Napenda pia kuwashukuru waliotoa Tribute kwa Kanumba kwa nyimbo na ujumbe mzuri wa kufariji na kumpa pongezi kwa kazi nzuri aliyoifanya katika baadhi ya foundations kusaidia watoto yatima, kukuza vipaji vya sanaa kwa waigizaji nakadhalika. Mungu aendelee kuwapa moyo huo huo wa ushirikiano Watanzania wenzangu. 
Maisha ni matamu ila mafupi, hatujui saa wala dakika tutakayoweza kuitwa, ningeomba tushirikiane kwa kuleta amani na kuwa na upendo kama kaka yetu marehemu Kanumba alivyo tuonyesha kwa wale wote walioguswa na kuhudhuria mazishi yake. Tuwasamehe wote waliotukosea na tumuweke mungu mbele na sala ziwe ndio wito wakutuongoza kila siku. Mungu awe nanyi na pia tusisahau kuiweka familia ya mdogo wetu LULU katika maombi, mungu awaongoze wanasheria katika kufikia maamuzi yatakayokuwa ya haki na kuleta muafaka katika familia hizi mbili. Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...