Search This Blog

June 19, 2012

KUTOKA FACEBOOK IMEANZISHA NA TG: PATA MUONEKANO WA BAJETI KIVULI.......


NAPE NNAUYE.....
HUU NI UUNGWANA KAKA ZITTO! HONGERA SANA!

"Maelezo ya Bajeti Kivuli
Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.

JUMLA YA MAPATO YA NDANI
Tshs. Millioni 11,889,078/-

MAPATO YA KODI
Tshs. Millioni 10,232,539/-

MAPATO YASIYO YA KODI
Tshs. Milion 1,163,533/-

MAPATO YA HALMASHAURI
Tshs. Milioni. 493,006/-
Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli wa Fedha

Kwa habari murua na mchakato wa wananchi tembelea.... https://www.facebook.com/nape.nnauye

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...