Search This Blog

December 9, 2012

VIGOGO WANAUSHIRIKIANO MAGAZETINI WANAUADUI......HAYA WASOMAJI WETU TOENI MAONI YENU!!!!!!

Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wanasiasa nchini wamekuwa wakitajwa kuwa ni maadui lakini kwa nyakati tofauti wamekuwa wakikutana na kuzungumza kwa furaha huku wakifotolewa, hali inayofanya wachunguzi wa mambo  kujiuliza huo uadui wao  upo wapi?
Wanasiasa wanaotajwatajwa kuwa wana uadui ni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Rais Jakaya Kiwete ambaye hata hivyo, Lowassa amewahi kuwashushua wanaowahusisha na uadui pale aliposema chanzo cha urafiki wao hawakukutana barabarani.
Aidha, Lowassa pia amewahi kutajwa kuwa na uadui na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samweli John Sitta hasa lilipolipuka suala la kujivua gamba ndani ya chama.
Sitta uadui wake na mwanasiasa huyo unaunganishwa na alipokuwa spika wa bunge kwa kuruhusu chombo hicho kuchunguza suala la Richmond, ambapo baadaye ilibidi Lowassa ajiuzulu uwaziri mkuu.
Alipopewa nafasi na Sitta
 kuzungumza  bungeni baada ya ripoti ya kamati ya bunge, Lowassa  alisema  kwamba kilichokuwa kikionekana katika sakata zima ni cheo alichokuwanacho, hivyo akaamua kuachia wadhifa huo mzito serikalini.

Source: GP

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...