Search This Blog

December 10, 2012

HONGERA RAISI WETU JK KWAKUOKOA MAISHA YA MWANAMZIKI RAY C KWA KUGARAMIA MATIBABU YAKE.


Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu, alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa pili kulia), Mama yake mzazi Ray C, Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.
---
Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.
Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake, Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
(Picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...