Search This Blog

December 9, 2012

SHEREHE ZA MIAKA 51 YA UHURU WA TANZANIA ZAFANA JIJINI DAR


Rais Jakaya Kikwete wakati akiwasili katika Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya sharehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania leo.
Rais Kikwete akipokea heshima ya mizinga 21 kutoka kikosi cha mizinga cha JWTZ.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika Uwanja wa Uhuru tayari kwa sherehe za miaka 51 ya uhuru wa Tanzania leo.
Rais wa Zimbabwe, Bi. Joyce Banda akiwasili katika Uwanja Uhuru kwa sherehe hizo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda naye akiwasili katika sherehe hizo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema akiwasili uwanjani hapo.
Kikosi cha bendera kutoka JWTZ kikijiandaa kwa ajili ya paredi.
Mwanajeshi akiokota silaha iliyovunjika wakati wa paredi.
Ofisa wa Polisi akiongoza paredi kwa ukakamavu.
Gadi ya wanawake kutoka JWTZ ikitoa heshima mbele ya viongozi waliohudhuria sherehe hizo.
TANZANIA leo imesherehekea miaka 51 ya uhuru ambapo viongozi mbalimbali kutoka nchi rafiki wamehudhuria sherehe hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika sherehe hizo, Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa mgeni rasmi ambapo  aliwashukuru viongozi wote waliohudhuria katika sherehe hizo.
Viongozi zaidi ya kumi kutoka nchi jirani waliweza kuhudhuria na kupata burudani ya ngoma za ndani na nje ya nchi.
(PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA / GPL)

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...