Search This Blog

May 22, 2012

MAUTAMU KUTOKA GLOBAL PUBLISHER'S YALIYOTANDA MAGAZETINI.....MLIO NJE YA NCHI PATA KUSOMA KISA NA MKASA......

Nimenukuuuu kama ilivyoandikwa kwa global publisher; 
"Stori: Makongoro Oging na Haruni Sanchawa

MUME wa msanii maarufu wa filamu nchini, Jack Patrick, Abdulhatif Fundikira anasakwa na polisi kwa madai kuwa anauza dawa za kulevya ‘unga’.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Fundikira anasakwa baada ya mwanamke mmoja Mariam Mohamed Saidi,29, kudakwa na polisi wa Kitengo cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini ambapo amemtaja Fundikira kuwa ndiye mwenye dawa alizokamatwa nazo ambazo ilikuwa azisafirishe kuzipeleka Uturuki.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa polisi walifika nyumbani kwa Fundikira saa 10 usiku wiki iliyopita lakini wakaambiwa kuwa hakuwepo, alikwenda kwenye msiba wa ndugu yake mikoani.
“Lakini hata mke wake hawakumkuta na hata walipopigiwa simu, zikawa hazipatikani na inavyoonesha wamepata fununu za kutafutwa na polisi hivyo kujikuta katika hali mbaya kila upende, wa dola na hata jamii,” kilisema chanzo chetu.
Gazeti hili lilimtafuta Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu madai hayo naye alikiri kujua tukio hilo.
Akasema vigogo wa mtandao wa dawa za kulevya wamejulikana na kilichobakia ni kufuatilia nyendo zao na kuwadaka mmojammoja.
Akizungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita ofisini kwake, Nzowa alisema kwamba orodha yao ni ndefu na kwamba Mei 16, mwaka huu kigogo mmoja akiwa na mke wake huko maeneo ya Buguruni Malapa wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam walitoroka kwao baada ya kupata taarifa kwamba mfanyakazi wao anayewasafirishia ‘unga’ nchi za nje,Mariam Mohamed Said ,29, amekamatwa.
Kamanda Nzowa amesema kwamba Mariam alikamatwa Mei 16, saa 9 usiku, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kilo 10 za bangi zenye thamani ya shilingi milioni 12 zilizofichwa kwenye sanduku ambapo mtuhumiwa huyo amedai kwamba amekua akifanya biashara ya baibui.
“Uchunguzi unaonesha kuwa inawezekana isiwe ni biashara ya bangi tu bali hata aina nyingine ya dawa za kulevya wamekua wakisafirisha,” alisema.
Mariam alikamatwa akiwa na bangi mabunda 23 yaliyofungwa kitaalam wakati akijiandaa kupanda ndege ya kwenda Uturuki na alionyesha nyumba ya kifahari ambayo ina chombo maalum cha kunasa picha, CCVT.
Kamanda Nzowa alifafanua kwamba Mariam atafikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi ukikamilika.
Hata hivyo, alikataa kutaja majina ya vigogo waliotoroka kwa madai kuwa ataharibu uchunguzi na amewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi.


Stori: Elvan Stambuli na mitandao
AINA moja ya dawa iliyothibitishwa kuwa ni kiboko ya Ukimwi na uwezo wa kuzuia maambuzi ya virusi ya Ukimwi (HIV), imepiga hatua muhimu ya kukubalika kutumika nchini Marekani.
Jopo la madaktari washauri wa serikali ya Marekani wameidhinisha matumizi ya dawa hiyo aina ya Truvada kwa watu walio katika hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya HIV.
Dawa hiyo, Truvada imekuwa ikitumika nchini humo na watu walio na virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2004 lakini ilikuwa haijaidhinishwa.
Utafiti umeonesha kuwa dawa hiyo inaweza kuwakinga watu wasiokuwa na virusi hivyo dhidi ya maambukizi.
Truvada ilianza kutajwa na kuandikwa katika vyombo vya habari nchini Marekani mwaka 2010 baada ya watafiti wa serikali kugundua kuwa inaweza kuzuia maambukizi ya HIV.
Utafiti wa miaka mitatu umebaini kuwa utumiaji wa dawa hiyo ambayo ipo katika muundo wa vidonge, ili kumkinga mtu na maambukizi, mtumiaji atapaswa (hasa mashoga ambao wapo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi), watatakiwa kumeza vidonge hivyo kila siku.
Utafiti wa mwaka jana uligundua kuwa Truvada ilipunguza maambukizi kwa asilimia 75 nchini humo baada ya kufanyiwa uchunguzi watu ambao ni patna ambao mmoja alikuwa na maambukizi.
Nick Literski, mfanyakazi katika shamba moja nchini humo ambaye mpenzi wake ana HIV alipofanyiwa utafiti kwa mwaka mmoja aligundulika hajapata maambukizi na alikuwa akilipa Dola za Kimarekani 40 (T sh. 64,000) kwa mwezi, bei ambayo imeonekana kuwa ingefaa kutumika.
Hata hivyo, sasa dawa hiyo inauzwa kwa dola za Kimarekani 900 (Tsh. 1,440,000) kwa dozi ya mwezi mmoja na kwa wale ambao watanunua kwa mwaka itawabidi watoe dola za Marekani 11,000 (T sh.11,600,000) hivyo kusababisha taasisi moja nchini humo iitwayo The AIDS Health Care Foundation kupinga gharama hizo na kudai
 kuwa ni kubwa mno.
Inakadiriwa kuwa watu milioni 1.2 nchini Marekani wana maambukizi ya HIV.


Na Imelda Mtema
"ALIMCHUKULIA kama shemeji, akamwamini kumbe kaka mtu alikuwa akishughulika ipasavyo na dada yake. Ilibaki siri nzito mpaka alipogundua Mei 15, mwaka huu na kufanya mauaji ya kutisha..."
Hivi ndivyo alivyoanza kusimulia mdogo wa marehemu Juma Matimbwa, Salum Shemtumba alipozungumza na mwandishi wetu wiki iliyopita.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Kimara Machungwa jijini Dar es Salaam hivi karibuni baada ya mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Mazengo kumuua kwa kisu, Juma Matimbwa na kumjerui vibaya hawara yake Angelina Michael, baada ya kuwafumania wakiwa wanavunja amri ya sita ya Mungu.
Akielezea sakata zima Shemtumba, alisema tukio hilo lilitokea Mei 15, mwaka huu maeneo ya Kimara King’oko baada ya Mazengo kupata habari kuwa shemeji yake Juma ana uhusiano na dada yake ambaye ndiye mpenzi wake.
Mtoa habari wetu huyo alizidi kuweka wazi kuwa baada ya kupata habari hiyo kutoka kwa watu wa karibu, akaanza kuzifuatilia kwa kina kama zina ukweli wowote huku akiandaa mtego wa kuwakamata mtu na dada yake ambao ni binamu ili kuweza kujua ukweli.
ALIVYOWAFUMA
Shemtumba alisema siku hiyo ya tukio Mazengo alifanikiwa kuwakuta chumbani Juma na Angelina baada ya kupata taarifa saa 6 mchana kutoka kwa wapambe kuwa shemeji yake huyo alifika nyumbani hapo na kuendelea kujivinjari na mpenzi wake(dada mtu).
“Kabla hajafika alikwenda nyumbani kwake ambako alichukua kisu na kuja kuwavamia,” alidai Shemtumba.
Aliongeza kuwa baada ya kuwafumania alianza kumkata sehemu mbalimbali za mwili Juma (marehemu) huku akimshambulia mpenzi wake kwa kisu tumboni na kichwani.

Aliendelea kusema kuwa baada ya Angelina kuona anashambuliwa, aliamua kukimbia na kujificha huku damu zikimtoka kwa wingi mpaka watu walipokuja sehemu ya tukio na kuanza kuamulia ugomvi huo ambapo Juma alikuwa ameshafariki kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kukatwakatwa kwa kisu mwilini na Mazengo alielekea kituo cha polisi kujisalimisha.
“ Baada ya Mazengo kufanya mauaji tu alienda kujisalimisha mwenyewe Kituo cha Polisi cha Kimara ambapo askari waliamua kumhamishia kituo kikubwa cha Mbezi kwa Yusufu,” alisema.
ANGELINA ASIMULIA
Gazeti hili lilienda mpaka nyumbani kwa Angelina ambapo lilimkuta ndiyo anatoka Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa na akajitetea kuwa yeye hakuwa na uhusiano na Juma kwa vile ni kaka yake na alikuja pale kwa lengo la kumsalimia tu na si vinginevyo.
Angelina aliongeza kuwa siku ya tukio alikuwa na kaka yake hapo nyumbani kwake kwa kuwa anauza pombe za kienyeji na kaka huyo alikuwa akinywa.
Baada ya muda mfupi waliongozana hadi kwenye kibanda cha Tigo Pesa kw ajili ya kuchukua fedha ili amlipe baada ya kupata kinywaji.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kurudi nyumbani alikuja Mazengo na kuanza kutukana bila kujua alikuwa na kisu na kuanza kuwachoma na kufanikiwa kumuua kaka yake kisha kumgeukia yeye na kumchoma tumboni.
Alisema aliamua kukimbia nje ili kujinusuru maisha yake.

“ Mimi kwa kweli namshangaa sana Mazengo kwa kuwa sikuwa na uhusiano wowote na marehemu Juma kwa vile alikuwa ni kaka yangu kabisa na mara nyingi alikuwa akija nyumbani kwangu na yeye alikuwa akimfahamu,” alisema Angelina akiwa katika maumivu makali.

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...