Search This Blog

April 2, 2013

WILLIAM RUTO: RAISI KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA WILLIAM RUTO MBUGANI SERENGETI.


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuongoza kuelekea kwenye chakula cha mchana  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto na mkewe Rachel Chebet katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara jana. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na familia ya  Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya, Mhe. William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara jana. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa  Naibu Rais mteule wa Kenya, Mhe. William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara jana. Mhe. Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara jana. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
(PICHA NA IKULU)
---
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS WA KENYA  WILLIAM RUTO MBUGANI SERENGETI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe. William Kipchirchir Samoei arap Ruto  ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Kitalii ya Seronera iliyoko katika mbuga ya wanyama ya Serengeti  mkoani  Mara, Rais Kikwete  amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimuelezea Mhe Rutto  juu y furaha yake pamoja na kuridhishwa  na jinsi  uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi hiyo.
Alielelezea  matumaini yake ya kuwa  urafiki uliopo kati ya Tanzania na Kenya  utadumishwa  pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani  Mara wiki  iliyopita akiwa na mke wake na watoto, ameondoka  leo baada ya chakula cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.
SOURCE: GP

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...