Search This Blog

April 18, 2013

VODACOM - Utoaji Wa Huduma Kwa Wateja Sekta Ya Mawasiliano Wazidi Kukua‏


Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akitoa huduma kwa wateja waliofika wakati wa uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja lililoko katika mtaa wa India Posta jijini Dar es Salam, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.

Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akimkabidhi funguo, Meneja Miradiwa Vodacom Tanzania, Sharon Rwekola, mara baada ya kuzinduliwa kwa duka jipya la kampuni hiyo lililoko mtaa wa India posta jijini dar es Salaam, Maduka hayo yanatarajiwa kupunguza msongamano kwa wateja wa kampuni hiyo.

•           Vodacom yazindua Maduka Mawili ya huduma kwa wateja.

•           Watanzania zaidi kuendelea kupata huduma za mawasiliano.

Dar es Salaam, April 18, 2013 … Huku jiji la Dar es Salaam likiendelea kukua kwa kasi na kushududia ongezeko kubwa la watu kutoka sehemu mbalimbali, upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii umekuwa ukikabiliwa na changamoto kadhaa kutokana na kasi ya utoaji huduma kutoendana na kasi ya ongezeko la watu.
Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, akitoa huduma kwa wateja waliofika wakati wa uzinduzi wa duka jipya la huduma kwa wateja lililoko katika makutano ya barabara ya morogoro Posta jijini Dar es Salam, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.
Meneja wa Duka la Vodacom lililoko mtaa wa Morogoro Posta Jijini Dar es Salaam, Sayed Shadab, mapema baada ya uzinduzi wa duka hilo, anayeshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Usambazaji na mauzo wa Vodacom Tanzania, Hassan Salleh, Vodacom imezindua maduka mawili yanayotarajiwa kupunguza msongamano katika maduka mengine ya kampuni hiyo.
Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Umma wa Vodacom Tanzania, Joseline Kamuhanda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.
Hivi karibuni wakazi wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dra es Salaam walishududia utolewaji wa elimu kuhusu mfumo wa mawasiliano wa 3G na 4G mfumo ambao unatumia teknolojia mpya ya mawasiliano kazi iliyofanywa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Baadhi ya wananchi waliofikiwa na kampeni hiyo ya utoaji elimu walitoa wito kwa serikali kushirikiana na wadau wengine wa teknolojia na mawasiliano kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya teknolojia na mawasiliano pamoja na matumizi sahihi ya huduma hizo.

Katika kukidhi haja hiyo ya utoaji wa huduma kwa wateja na elimu kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeendelea kupanua wigo wa huduma kwa kufungua maduka mawili yatakayo endelea kutoa huduma kwa wateja na kufanya mauzo ya bidhaa mbalimbali katika mtaa wa India na barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia wakati wa uzinduzi wa maduka hayo, Mkuu wa kitengo cha Mahusiano ya Umma, wa Vodacom Tanzania Joseline Kamuhanda, amesema Vodacom ni kampuni pekee ambayo imeendelea kuongoza kwa kuwa na maduka mengi ya mauzo na huduma kwa wateja kwa kufikisha maduka 65 ikiwa ni kampuni pekee kuwa na maduka mengi ya huduma na kufanikisha adhma ya kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wa kampuni hiyo huku Dar es Salaam ikiwa na idadi ya maduka 20.

“Ukuaji wa huduma kwa kampuni ya Vodacom umekuwa mkubwa sana, huduma kama ya M – Pesa sasa imepanuka kwa kasi na sasa inatoa huduma kwa watanzania zaidi ya milioni 10. Kufuatia mafaanikio haya tunalazimika kuhakikisha upatikanaji wa huduma kwa wateja  ni wa uhakika” alisema Kamuhanda na kuongeza kuwa,

“Kuongoza katika sekta ya mawasilaino kuna changamoto zake, lazima tuhakikishe tunaendana na kasi ya ukuaji na ongezeko la watu na uhitaji wa huduma zetu kwa watu wa aina mbalimbali.

Aidha Kamuhanda alisema kuwa Kufunguliwa kwa maduka hayo sasa sio tu kunaboresha upatikanaji wa huduma pia ni fursa pekee ya kuendelea kupanua wigo wa ajira kwa watanzania.

“Ufunguzi wa maduka haya unatoa fursa ya ajira kwa Watanzania, Ufunguzi huu umejumuisha na ajira kwa wafanyakazi 10 ambao watatoa huduma kwa wateja wetu hivyo ni hatua kubwa tumetengeneza ajira kwa wafanyakazi wapya. Hadi kufikia sasa, Vodacom imetoa ajira za moja kwa moja kwa wafanyakazi 500 na wengine zaidi ya 30,000 wenye ajira zisizo za moja kwa moja,”
SOURCE: GP

No comments:

Post a Comment

ABUSIVE LANGUAGE IS NOT ALLOWED TO THIS BLOG. THANK U FOR UR COOPERATION

Note: Only a member of this blog may post a comment.

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...