Search This Blog

August 27, 2012

DMK: CCM ILIVYOFUNIKA DMV-OFFICIAL VIDEO ON THE WAY.


HATUWEZI ISHI BILA CCM KUBALINI KATAENI CCM NDICHO CHAMA PEKEE..........
 Wanachama wa CCM walifurika mpaka kukakosekana pa kukaa, jaamani kwa upande wangu nibora kujiunga katika chama tukufu na tuweze kushirikiana kutatua matatizo yaliyopo na kuweza kuendeleza maendeleo kwa wana jamii. Kwamliokosa mlikosa tukio la kihistoria kwakweli, jitahidini kuweza kuhudhuria uzinduzi mwingine ujao hivi karibuni, nitawapatia maelezo zaidi hivi karibuni.
 


August 24, 2012

DIAMOND NDANI YA MAREKANI.........


Stori: Sifael Paul
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.
Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.
“Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani.
“Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
Source: GP

YOU MAY ALSO LIKE THIS

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...